Safari kwenye misitu
ya Afrika
Hifadhi ya Taifa ya Gombe ni makazi ya jamii ya sokwe wanaoishi porini kuwahi kufanyiwa uchunguzi wa kina. Zaidi ya miaka 50 iliyopita, Dk. Jane Goodall alianza kazi yake hapa, na historia ya ugunduaji wa sayansi inaendelea hadi leo. Angalia kwa karibu.
Kuwaelewa na kuwalinda sokwe
Miaka ya utafiti
54
SAA ZA UCHUNGUZI
200,000
Historia kamili za maisha
40
Tunapotembea msituni tunakutana na Glitter na binti yake Gossamer akiwa
mgongoni pake. Sokwe kina mama kwa kawaida huwa na kati ya watoto 4 na 6,
kukiwa takribani miaka 5 kati ya kila mtoto. Pacha huwa nadra, ingawa Glitter
mwenyewe ni pacha. Sokwe wachanga huishi miaka 10 ya kwanza ya maisha na mama
zao, na kwa miaka 3-4 ya kwanza wao hupata safari za kubebwa mgongoni na
begani hivi.
Talii eneo hili
Sokwe huyu ni sehemu ya Familia ya G, na ana jina rahisi kukumbukwa: Google.
Alitajwa jina hilo kwa heshima ya ushirikiano wa muda mrefu kati ya JGI na
Google, sokwe huyu ni sehemu ya jamii ya Kasakela, mojawapo ya jamii tatu za
sokwe walio Gombe. Ingawa wanaweza kuwepo zaidi ya sokwe 160 katika jamii,
wao hupenda kutumia muda wao wakiwa peke yao au katika vikundi vidogo
sana.
Talii eneo hili
Sokwe hutumia takribani saa saba kwa siku wakila, na ikiwa hawali
wanapumzika, kucheza na kusafishana. Ni wanyama wanaopenda ujamaa sana, na
huwasiliana kwa kiwango kikubwa sawa na wanadamu wafanyavyo: kwa kubusu,
kukumbatia, kutekenya na kushikana mikono. Pia hupiga kelele na kugonga miguu
yao chini kama sisi! Nyakati za usiku sokwe hujenga viota vya kulala
mitini.
Talii eneo hili
Siku katika maishani ya sokwe
Maisha msituni yako vipi? Barizi na sokwe wa Gombe kama vile Glitter na Gossamer
na
ujifunze kuhusu tabia za viumbe ambao
98% ya DNA yao ni sawa na yetu.
Kutana na viumbe wanaoishi Gombe
Sawa na misitu yote, Hifadhi ya Taifa ya Gombe ni
mfumo maalum wa ikolojia ulio na viumbe wa
maumbo na ukubwa wote. Wajue majirani.
Sokwe
Sokwe wa kawaidaSokwe
Sokwe wa kawaida
Kusimama wima! Ingawa sokwe wanaweza kusimama kwa miguu yao ya nyuma, wao hutembea kwa miguu minne wakiwa wamekunja ngumi . Wana mikono iliyo miepesi kukunjika na gumba kama za binadamu, lakini pia wana vidole virefu na vidole vikubwa vya miguu vinavyowawezesha kushikilia matawi ya miti wanapotafuta chakula.
Nyani
Papio anubisNyani
Papio anubis
Rafiki au adui? Ingawa nyani na sokwe hucheza pamoja utotoni, wanapokua urafiki kati yao huanza kupungua. Mara nyingi nyani hutafuta vyanzo sawa vya vyakula kama sokwe, na sokwe huwala watoto wa nyani. Tofauti na sokwe, nyani hupende kuogelea, kurusha na kucheza ndani ya maji.
Bafe wa Kichakani
AtherisBafe wa Kichakani
Atheris
Kuwa makini unapotembea! Katika magugu yaliyoenea ardhini unaweza kumwona nyoka huyu wa sumu mwenye magamba anayepatikana katika msitu wa Gombe. Sokwe wana woga na silika kama ya binadamu kuhusu nyoka. Hata wana mwito maalum ('wraa ya nyoka') unaowaarifu sokwe wengine kwamba kuna nyoka msituni.
Mende wa samadi
SkarabiidiMende wa samadi
Skarabiidi
Kutana na mrejelezaji hodari. Mende hawa hubiringiza vinyesi na kuunda mipira midogo wanayoizika na kutaga mayai ndani yake, na hata kuunda makazi nayo. Wadudu hawa ni muhimu sana katika mfumo wa ikolojia, ikiwa ni pamoja na kutawanya mbegu na kupenyezavirutubisho katika udongo .
Jongoo
SpirostreptidaJongoo
Spirostreptida
Ina miguu! Majongoo hujulikana kwa miguu yao mingi wanayotumia kutembea katika ardhi ya msitu, wanaposaidia kutenganisha miti, kuvu, wanyama na vidudu vinavyooza. Miguu ya arthropoda huyu huwa muhimu pia katika taratibu zake za uchumba.
Hifadhi ya Taifa ya Gombe ni eneo linalolindwa lililo kwenye mpaka wa
magharibi ya Tanzania. Ikiwa karibu na fukwe za Ziwa Tanganyika, mbuga hii ni
mchanganyiko wa nyika na misitu ya kupukutika, na misitu ya kijani daima.
Katika misitu ya Gombe wanaishi sokwe waliofanyiwa utafiti wa muda mrefu
zaidi Duniani.
Talii eneo hili
Sokwe ni wenyeji wa misitu ya Afrika ya Kati na Magharibi, ikiwemo Tanzania.
Wanaishi karibu na miti kwa sababu chakula chao msingi ni matunda, ingawa
wanapenda majani, wadudu na mamalia wadogo (wakiwemo tumbili). Ukitembea
kwenye msitu wenye sokwe utasikia mito na majibu ya mikoromo na ukwenzi.
‘mikoromo’ hiyo ndizo sauti wanazotumia sokwe kujitambulisha na
kuwasiliana na wengine.
Talii eneo hili
Mnamo 1957, Jane Goodall akiwa na umri wa miaka 23 alihamia Afrika Mashariki
kutoka nchi yake ya Uingereza ili kufuatilia mapenzi yake ya utotoni kwa
wanyama wa Afrika. Alimfanyia kazi mtafiti maarufu wa visukuku Louis Leakey,
aliyeamini kuwa utafiti wa nyani ungaliweka wazi taarifa kuhusu mababu wa
zamani wa wanadamu. Moyo wa ujasiri wa Jane ulimwelekeza katika misitu ya
Gombe Julai 1960, lakini utafiti wake wa uvumbuzi hapa ndio uliobadilisha
mwelekeo wa elimu kuhusu sayansi ya kisasa ya mamalia.
Talii eneo hili
Jane alipohamia Gombe mara ya kwanza, aliishi hemani na mama yake, akafanya uchunguzi wake akitumia darubini iliyowahi kutumiwa na kuandika madokezo kwa penseli na karatasi. Alitazama walichofanya sokwe siku nzima, akiandika kuhusu tabia na miundo yao ya jamii ya kila siku. Baadaye alitambua kuwa uchunguzi aliokuwa akiufanya ulikuwa tofauti na dhana nyingi za kawaida kuhusu sokwe.
Mara ya kwanza sokwe walikuwa wanamwogopa sana Jane, na ilikuwa vigumu kufanya utafiti. Baada ya muda wakazoeana, au wakamzoea, na akaweza kuwatazama kwa ukaribu, na hata kuingiliana nao. Alishuhudia sokwe wakicheka, wakicheza, wakisafisha manyoya, wakitafuta chakula na kuwinda. Pia alishuhudia vurugu zao, na hata kushuhudia vita vya sokwe . Kwa kuishi nao porini, Jane alikuwa akifichua ulimwengu wa siri wa sokwe.
Katika mwaka wake wa kwanza, Jane alimchunguza sokwe aitwaye David Greybeard akitumia nyasi kutoa mchwa kutoka mashimo madogo. Alikuwa akitumia nyasi kama kifaa, kitu ambacho wanasayansi waliamini kilikuwa cha kipekee kwa wanadamu. Uchunguzi wa Jane ulibadilisha fikra zetu kuhusu uhusiano kati ya wanadamu na wanyama. Sasa tunajua kuwa sokwe ni jamaa wa karibu wa wanadamu, walio na 98% ya DNA sawa na yetu.
Jane alikuwa mtafiti asiye wa kawaida wa wanyama, hivi kwamba aliwapa majina wanyama wake badala ya kuwapa nambari. Alianzisha mfumo wa kutoa majina ambapo watoto wanapewa majina ambayo yanaanza kwa herufi sawa na jina la mama yao. Shajara ya familia inaonyesha aila ya G-Family, ambao ni sehemu ya jamii kubwa ya sokwe wa Kasakela. Google, Glitter na Gossamer sasa wanaweza kuonekana katika Street View.
Mwaka wa 1977 Taasisi ya Jane Goodall ilianzishwa ili kuendeleza utafiti uliopo Gombe, na kupanua ufikiaji wa kazi ya kisayansi ya Jane na maono ya kuimarisha maslahi ya binadamu. Leo dhamira ya JGI inalenga zaidi ya Gombe, kwa kuwa shirika linajitahidi kulinda 85% ya sokwe na makazi yao kote Afrika. Pia wanahusisha vijana kote duniani katika miradi ya uhifadhi wa jamii kupitia mpango wa Roots na Shoots.
Wanasayansi katika Kituo cha Utafiti cha Mto Gombe wanashirikiana na maabara kote duniani, ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Duke , kuchangia masomo ya kitaaluma. Wakitumia misusruru ya utafiti uliofanywa Gombe kama takwimu za msingi, wanasayansi wanaweza kutabiri jinsi mabadiliko katika mazingira, miundo ya kijamii, na magonjwa yanavyoweza kuathiri idadi ya sokwe pakubwa. Kuwatafiti sokwe pia kunaweza kufichua maelezo kuhusu wanadamu (k.m., utafiti kuhusu SIV miongoni mwa sokwe wa Gombe umechangia kutafiti virusi vya UKIMWI).
JGI pia imewekeza katika mpango wa uhifadhi wa jamii unaowawezesha watu kujenga maisha yao ya kudumu huku ikiimarisha malengo ya uhifadhi wa eneo, kama vile upandaji miti na kukomesha biashara ya nyama pori. Kwa kuwekeza katika afya na elimu, na kutoa mafunzo katika usimamizi wa rasilimali, kilimo na elimu misitu, mipango ya uhifadhi unaozingatia jamii inaimarisha ukuaji wa uchumi na utamaduni huku ikilinda maliasili.
Kulinda sokwe kunamaanisha kulinda makazi yao, na makazi hayo ni zaidi ya mipaka ya hifadhi. JGI inasambaza simu mahiri na kompyuta kibao za Android zinazotumia GPS kwa watu wa karibu na wahifadhi mbuga kote Afrika. Wachunguzi hawa wa misitu wamewezeshwa kurekodi na kuripoti uwepo wa wanyamapori na shughuli haramu za binadamu kwenye vifaa. Kisha data inapakiwa katika wingu, kuchanganuliwa kwa kutumia Mtambo wa Google Earth na kushirikiwa na wafanyauamuzi.
Data ya nyanjani iliyoripotiwa na wachunguzi wa misitu inapounganishwa na picha ya setilaiti, wanasayansi wa uhifadhi wanaweza kuchunguza afya ya makazi ya sokwe kwa upana. Kwa kutumia teknolojia vumbuzi, wanasayansi hawa wanaweza kupanga, kutekeleza na kupima jitihada za uhifadhi wa makazi. JGI inashughulika ili kuboresha jitihada za kuchunguza misitu kwenye makazi yote ya sokwe ili kuruhusu maarifa ya karibu kufikiwa kimataifa.
Kwa mfumo wake wa ikolojia wa kipekee, idadi ya sokwe iliyowekwa katika kumbukumbu kwa uangalifu wa juu na zaidi ya miaka 50 ya utafiti wa kupigiwa mfano, Gombe ni maabara inayoishi. Ugunduzi uliofanywa katika misitu ya Gombe unatumika kwenye mifumo ya ikolojia kote duniani. Likiwa eneo lenye urembo asili, makazi muhimu ya wanyamapori na kitovu cha utafiti wa kisayansi, kwa kweli Gombe ni eneo lisilokuwa na mfano wake.
Historia ya utafiti
Gombe
Kabla ya uchunguzi wa Jane eneo la Gombe, iliaminika kuwa wanadamu ndio waliokuwa viumbe pekee Duniani waliotumia zana. Gombe imekuwa kitovu cha utafiti wa pekee tangu wakati huo, kikiongozwa na Taasisi ya Jane Goodall iliyoangazia sokwe, uhifadhi na jamii.
Ujumbe kutoka kwa Jane Goodall
Nilipoenda Gombe, nilipanga kuchunguza na kujifunza kuhusu sokwe wa kushangaza wanaoishi huko. & nbsp.; Nilichojifunza katika miaka yangu ya utafiti katika Gombe kilinitia moyo na kunijulisha mengi. Ninatumaini kwamba safari yako kupitia tovuti hii na picha za Street View itakupa ziara kama yangu ya kujifunza na ugunduzi.
Katika muda wangu niliokuwa Gombe na miaka iliyofuata, nilipata ujuzi wa moja kwa moja kuhusu umuhimu wa kila mmoja wetu kuelewa dunia tunamoishi. Kwa sababu tutakapoelewa vizuri ndipo tutakapoanza kujali, na tukianza kujali tutaanza kuchukua hatua. Hivi ndivyo mabadiliko hufanyika. Hivi ndivyo tutakavyofanya mabadiliko tunayohitaji ili tuishi kwa usawa na amani katika sayari hii tunayoiita nyumbani.
-Dk. Jane Goodall, PhD, DBE na Mjumbe wa Amani ya Umoja wa Mataifa,
Mwanzilishi wa Taasisi ya Jane
Goodall
Oktoba 21, 2014
Talii
Hifadhi ya Taifa ya Gombe
Gundua baadhi ya spishi nyingi zinazoishi
Gombe unapotembea kwenye njia za ufuo
na barabara za msituni katika Street View.