Jinsi Autori imebadilisha ukarabati wa barabara katika maeneo yote ya Ufini, kupitia picha moja baada ya nyingine katika Taswira ya Mtaa.

Ubora wa hali za barabara, ishara za zamani na mitaa isiyo na taa ni changamoto za kila siku kwa madereva na manispaa kote ulimwenguni. Lakini Autori, kampuni ya programu ya Kifini inayounda suluhu za ukarabati wa miundombinu, ilipata njia ya kukusanya na kuchambua data ya kiwango cha mitaa kwa ufanisi zaidi kwa kutumia Taswira ya Mtaa ya Ramani za Google.

Kilomita 40,000

picha zilizopigwa

Milioni nane

picha zilizochapishwa

Milioni 50

mara za kutazamwa

data kuhusu barabara

20

miradi ya kupiga picha

Kuboresha usimamizi wa ukarabati wa barabara nchini Ufini

Autori ilianzishwa mnamo 1988, na hutoa suluhu za Programu kama Huduma (SaaS) kwa mamlaka za barabara, wakandarasi na washauri wengine katika Ufini kuhusu usimamizi wa hali, upangaji wa hatua na uratibu wa ukarabati. Kufuatilia hali za barabara nchini kote kunachukua muda mwingi na hugharimu pesa nyingi. Japo kampuni zingine zilikuwa na wasiwasi kuhusu gharama, Autori iliweza kutumia fursa hii ya kipekee. Wakitumia picha zao za Taswira ya Mtaa na suluhu za SaaS, wameunda zana ya usimamizi bora wa data ya miundombinu ya ukarabati wa barabara na ya kufanya uamuzi nchini Ufini.

Umuhimu wa kasi na kushiriki data

Kwa kawaida, mamlaka za barabara zinapaswa kutembelea kila barabara ili kujua ni kazi gani inahitajika katika maeneo mahususi. Hii inamaanisha kuendesha kwa maelfu ya kilomita na kusimama mara nyingi ili kuandika maelezo. Shughuli hii haiathiri tu mazingira, bali ni ghali mno, inatumia nyenzo nyingi na inachukua muda mwingi. Kwa hivyo, umuhimu wa kupata suluhu ya dijitali ambayo haiathiri mazingira sana ilipelekea wataalamu wa Autori kuwa wabunifu zaidi. Na Taswira ya Mtaa ilikuwa suluhu ya kwanza ya taswira ya kiwango cha mtaa ambayo walizingatia.

 

Kupata maelezo kuhusu ukarabati wa barabara kunahitaji kushiriki mara nyingi kiasi kikubwa cha data na washirika mbalimbali. Taswira ya Mtaa ina zana zote muhimu za kufanya mchakato wa kushiriki maelezo uwe rahisi kati ya watumiaji - inapatikana kwa kila mtu aliye na simu mahiri na haihitaji uingie katika akaunti au usanikishe programu yoyote. Na ingawa Taswira ya Mtaa imekuwa ikitumika katika ukarabati wa barabara hapo awali, kuweka data iliyosasishwa ndiyo ilikuwa changamoto kubwa zaidi. Tuliona fursa ya kutatua tatizo hilo kwa kuunganisha Taswira ya Mtaa na programu yetu ya ukarabati wa barabara.

-

Ari Immonen, Mkuu wa kitengo cha Ushauri wa Mambo ya Dijitali katika kampuni ya Autori

 

Taswira ya Mtaa ya Google - Autori inaweka barabara za Ufini kwenye ramani

Kuunganisha juhudi za mtandaoni na za nje ya mtandao kwa usalama barabarani

Mapema mwaka wa 2017, kampuni ya Autori ilianza kupiga na kupakia picha za digrii 360 za barabara za serikali nchini Ufini, ikitumia akaunti ya Google ya kampuni yake ili kuchapisha picha. Tangu wakati huo, wamerekodi kilomita 40,000 za barabara za serikali na kupakia picha milioni 8. Hali hii imewezesha usimamizi wa ukarabati wa barabara mtandaoni. Kwa kuunganisha Taswira ya Mtaa na suluhu zao za SaaS wamefanya iwe rahisi kwa mamlaka za barabara kupata maelezo yaliyosasishwa ya rasilimali za barabara kwa mbali.

Kutokana na picha ambazo kampuni ya Autori imechapisha kwenye Taswira ya Mtaa, ripoti za ishara zinazokosekana, alama au mashimo barabarani zinaweza kupakiwa na kuwekewa lebo ili washirika husika waweze kuzikagua kutoka ofisini mwao kupitia dashibodi ya Autori. Kwa kutoa suluhu inayoweza kuwekewa mapendeleo, Autori pia inaruhusu wakandarasi kufuatilia na kupanga kazi inayofaa ya ukarabati wakiwa katika sehemu moja. Wakati kazi ya ukarabati imekamilika, picha mpya za digrii 360 za eneo hilo hupigwa na kupakiwa na wafanyakazi ili kusasisha data ya barabara. Hatua hii imepunguza hitaji la kutembelea eneo halisi kwa ajili ya ukaguzi - hivyo kuokoa muda, pesa na kupunguza uzalishaji wa gesi joto.

Kuimarisha usalama wa barabarani kila mahali

Taswira ya Mtaa iliruhusu Autori kuboresha mchakato wa kushiriki maelezo na kuhamasisha kuhusu hali kwa mamlaka za barabara nchini Ufini. Hali hii ilisaidia kupunguza gharama na kuongeza ufanisi. Huku ikitambua athari nzuri ambayo inaweza kuleta kote ulimwenguni, Autori sasa inajitahidi kubuni muundo maalum wa kukusanya na kushiriki data kuhusu barabara katika siku zijazo. Iliwasaidia pia wakazi kupunguza jumla ya kaboni kwa kupiga picha kilomita 1,000 za njia za baiskeli na za wanaotembea kwa miguu. Watu sasa wanaweza kupata data iliyosasishwa na kusafiri umbali mfupi kwa njia isiyo na athari kubwa kwa mazingira. Aidha, kampuni hii itarudi barabarani tena msimu huu wa kiangazi ili kukusanya picha za kilomita 15,000 zaidi nchini Ufini, na hivyo kukaribia kupiga picha na kuchapisha karibu nusu ya barabara zote za serikali nchini kwenye Taswira ya Mtaa.

Mafanikio ya Autori ni mfano mmoja tu wa njia nyingi za kipekee ambazo biashara zinatumia Taswira ya Mtaa ili kutatua matatizo.changamano. Ni zaidi ya zana ya kuweka ramani kwa kutumia picha na inaweza kuwa na manufaa mengi kwa biashara yako pia. Je, uko tayari kueleza habari yako ya mafanikio ya Taswira ya Mtaa?

Shiriki Picha zako mwenyewe za Taswira ya Mtaa