Tahadhari dhidi ya matukio ya ulaghai na matumizi mabaya
Jihadhari na wageni au anwani kutoka kwa wanaojitambulisha kama wafanyakazi wa Google, ambao hutoa aina mbalimbali za usaidizi na taarifa za picha au data za hali yoyote. Tunasisitiza kwamba kampuni hizi hazijaidhinishwa kuzungumza kwa niaba ya Google na ni lazima zijitambulishe kama makontrakta wa nje.
Tunakushauri kwa dhati kuwa wakati wowote ambapo mtu anawasiliana nawe kwa niaba ya Google moja kwa moja, tafadhali puuza mawasiliano kama hayo, haka kama yanalenga sababu zozote kama zile zilizotajwa hapa chini:
- Kutoa huduma au mafunzo kwa niaba ya Google, kuweka vipimo, maudhui ya kidijitali, kuripoti kuhusu mitindo ya kidijitali au mifumo mipya ya kidijitali na mitindo mipya ya biashara; ushauri wa maudhui, nk.;
- Kutoa ahadi ambazo hazilingani na utendaji wa kawaida wa huduma za Google, kama vile kuhakikisha kupata nafasi ya juu katika huduma ya Tafuta, Taswira ya Mtaa ya Google au Ramani za Google;
- Kushinikiza mshirika anayetoa kandarasi kwa kupiga simu za utangazaji au vitisho vya kuondoa maudhui kwenye mifumo ya Google.
Ni muhimu ukumbuke kuwa Google haiajiri wapigapicha au mawakala. Wataalamu hawa ni sehemu ya asasi za nje na majadiliano yote hufanywa bila kuhusisha wala kushirikisha Google.
Tunathamini sana usalama wa watumiaji. Kwa sababu hiyo, tunazuia matumizi ya chapa za Google na mifumo yake. Hakuna asasi iliyoidhinishwa:
- Kutumia chapa ya Google, kama vile aikoni, muhuri na/au nembo ya Taswira ya Mtaa kwenye magari ya kampuni;
- Kutumia chapa za Google, Ramani za Google na Taswira ya Mtaa au chapa nyingine za biashara za Google au vipengee kama hivyo katika jina la kikoa;
- Kutumia chapa za Google, Ramani za Google na Taswira ya Mtaa au chapa nyingine za biashara za Google au vipengee kama hivyo kwenye mavazi (sare n.k.);
- Kutumia chapa za Google, Ramani za Google na Taswira ya Mtaa au chapa nyingine yoyote ya biashara ya Google au vipengee kama hivyo, katika Wasifu wa Biashara zao kwenye Google;
- Kutumia chapa zozote za biashara za Google, kwa njia inayoonyesha kwamba Google imeidhinisha bidhaa au huduma mahususi.